SKENDO YA PICHA ZA UTUPU NA KUKATA MAUNO WANAKWAYA WAMVAA KOKETI,
AU BIASHARA MATANGAZO?
Kuna baadhi walidai labda mwanadada huyo anafanya hivyo ikiwa ni njia ya kujitangaza yeye na biashara yake bila kujali kama anaweza akajiondolea ute wake na heshima aliyoijenga kwa miaka mingi.
“Ukweli ni kwamba Jojo (Jokate) anatutia aibu maana malezi ya kidini hayapo hivyo. Anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na watu wote.
USHAURI WA BURE
“Sisi tunamshauri arudi awe kama zamani kwani alikuwa binti wa mfano kanisani. Hakuna mtu wa kuonesha maumbile yake muhimu hadharani. Kwanza alipoingia kwenye mambo ya muziki ndiyo hali imekuwa mbaya maana ukiona video zake hutamani kuziangalia na watu wenye heshima zao,” alisema mmoja wa wanakwaya hao kwa niaba ya wenzake huko akiomba chondechonde kutotajwa gazetini.
JOKATE AJITETEA
Akizungumza na Ijumaa juu ya sakata hilo, Jokate alifunguka kuwa, kanisa analosali halimzuii kukata mauno jukwaani kwani anachofanya yeye ni kazi kama kazi nyingine.Jokate ambaye ndiye mmiliki wa bidhaa za ‘brandi’ ya Kidoti alisema kwamba, huwa anakwenda kanisani kama kawaida na kwaya anaimba kama siku zote na hilo haliwezi kumzuia kufanya kazi yake ya muziki na kukata mauno.
MAUNO KWA WINGI YANAKUJA
Jokate alisema kuwa ngoma yake mpya aliyokuja nayo hivi karibuni ya Leo Leo aliyomshirikisha Ice Prince wa Nigeria ndiyo imemdatisha na watu watarajie mauno kwa wingi kwani amejipanga vilivyo.“Mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani mauno ya sasa si mchezo, ni hatari tupu, nimedata na huu muziki, kiukweli nitajiachia kuliko siku zote,” alisema Jokate ambaye pia ni mwigizaji wa sinema za Kibongo
No comments:
Post a Comment