Recent Post

Saturday, March 28, 2015

PATA TAARIFA KUHUSU Askofu Gwajima



Askofu Gwajima kaenda Polisi Dar es salaam jana, alichosema je? kiko hapa
gwajima
Miongoni mwa taarifa zilizochukua Headlines katika taarifa ya Habari ya kituo cha ITV ni hii ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima  ambae amefika kituo kikuu cha Polisi Dar kwa ajili mahojiano na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa kauli yenye maneno makali kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki, Askofu Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima amesema maneno aliyoyatoa ni ya kumkemea kiongozi mwenzake wa kiroho kwa madai ya kukiuka msimamo wa viongozi wenzie wa dini wa kukataa Mahakama ya Kadhi.
gwa (1)
Baraza la Maaskofu Tanzania waliamua kwa pamoja na wakasaini waraka kwa pamoja, kwamba hawataki Mahakama ya Kadhi… lakini tukashangaa mwenzetu Askofu Pengo aliyesaini na yeye anageuka sasa tukajiuliza kwa nini anageuka? mimi kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee.. lakini nimeitwa na Polisi sasa najiuliza niliyemkemea ni Polisi au nilimkemea nani? –Askofu Gwajima.
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumezagaa picha za video zenye maneno ya kashfa kwenda kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Askofu Kardinali Pengo jambo lililofanya jeshi la Polisi kumtaka afike kituoni  kikuu cha Polisi kwa mahojiano.
 

Email Newsletter



Smiley :)
:D
:)
:[
;)
:D
:O
(6)
(A)
:'(
:|
:o)
8)
(K)
(M)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Us

Contact Form

Name

Email *

Message *