Pichaz: Madonna, Nicki Minaj,Rihanna, Beyonce, Alicia Keys,Usher, Kanye West kwenye uzinduzi wa Tidal ya Jay Z
Jay ameamua kuendelea kuonyesha ni jinsi gani amewekeza katika himaya ya burudani duniani baada ya jana kuzindua kampuni yake mpya ya muziki inayojulika kwa jina la Tidal ambayo sasa atakuwa akinunua kazi za wasanii wengine na kuziuza kupitia kampuni hiyo.
Raper huyo katika uzinduzi huo uliofanyika New York aliamua kuwashirikisha wasanii wakubwa wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya muziki duniani ambao ndio waanzilishi katika kampuni hiyo.
Wasanii hao ni pamoja na Alicia Keys, Arcade Fire’s Win Butler na Régine Chassagne, Beyoncé, Daft Punk, Jack White, Jason Aldean, J. Cole, Kanye West, Deadmau5, Madonna, Nicki Minaj, Rihanna, Calvin Harris, Chris Martin na Usher.
Alicia Keys ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kwa ufupi kuwa lengo la kuungana ni kuhakikisha wanshirikiana kaika sauti moja na kuhakikisha wanaleta mapinduzi katika historia ya muziki kwa manufaa ya mashabiki na wasanii kwa ujumla.JAY-Z ALIEKUA AMEFULIA KWA KUNUNU KAMPUNI HIYO KWA GHARAMA KUBWASANA SASA AMEWEZA KUWASHAWISHI WASANII HAO NA HATIMAYE ANARUDI KUKAMATA LINE KIMKWANJA
No comments:
Post a Comment