Recent Post

Tuesday, March 31, 2015

PNC na ishu ya Ostaz Juma, video ya Diamond kwenye TV na alichokisema Babu Tale



PNC na ishu ya Ostaz Juma, video ya Diamond kwenye TV na alichokisema Babu Tale.. #255

entertainmentKuna story iliyoenea kuwa aliyekuwa Meneja wa kundi la Watanashati, Ostaz Juma kuwa amefilisika, 255 imepiga story na msanii ambae aliwahi kusimamiwa na  Meneja huyo, PNC ambae amesema alisikia taarifa hizo na amewahi kuhojiwa lakini hajui kama ni kweli.
PNC amesema watu wanahisi kwamba amemfanyia kitu kibaya kwa imani za kishirikina, lakini lakini sio kweli na hajui kilichosababisha awe katika hali hiyo.
dp5Wiki iliyopita msanii Diamond Platnumz aliachia video ya wimbo wake mpya wa‘Nasema Nawe’ aliomshirikisha Khadija Kopa katika mtandao wa Youtube na leo alipanga kuuachia kwenye vituo vya Television, Diamond amesema ameamua kusimamisha kutokana na msiba wa kiongozi wa kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge.
IMG_7570Story ya mwisho kusikika inahusu msiba wa mwanzilishi wa kundi la Tip Top ConnectionAbdul Bonge, kwenye 255, Babu Tale ambae ni mdogo wa Marehemu amesema kuna rafiki yao alikuwa anagombana na mke wake akaja mtu kumuomba Abdul akasaidie kuumaliza ugomvi huo.
Tale amesea Marehemu alikataa kwenda kwenye ugomvi huo, baadae akaamua kwenda kusaidia, muda mfupi baadae alikuja mtu kumuita kaka yake mwingine na kumwambia amfate kaka yao amezimia kutokana na kusukumwa wakati anaamulia ugomvi huo, walipompeleka Hospitali wakaambiwa ameshafariki, leo mwilli wake umesafirishwa kwenda Morogoro kwa ajili ya mazishi.
#RIP #AbdulBONGE

Email Newsletter



Smiley :)
:D
:)
:[
;)
:D
:O
(6)
(A)
:'(
:|
:o)
8)
(K)
(M)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Us

Contact Form

Name

Email *

Message *