
Zilizosikika kwenye 255 leo ipo inayomhusu 
Fredrick Bundala ambae amekuja na kitabu kinachozungumzia maisha ya 
Mtemi Mirambo wa Tabora, akizungumzia kitabu hicho amesema ni  idea  iliyozoeleka nchi za nje na baada ya kupitia mitandao akagundua Audio box  kwenye soko ni kitu kikubwa sana na anapenda sana kusimulia matukio kama alivyowahi kufanya katika documentary kuhusu Mv Bukoba akaona anauweza kufanya kitu kwa kusimulia na watu wakakipenda akatengezena kitabu katika mfumo wa sauiti (Audio Box) kinachoitwa 
Mtemi Mirambo (Sultani Mkuu wa Afrika)

Baadhi ya wasanii wameonekana kuhamia kwenye siasa kama 
Mr Two, 
Prof. Jay, 
Afande Sele na wengine msanii 
Juma Nature amesema alikuwa amepanga kufanya hivyo na watu walimfata ila mwa mkwa huu ameona asigombee, kama angegombea Ubunge Temeke angepita ila kwa sasa amewaachia wasanii wenzake, ikitokea akawa Mbunge jambo la kwanza kufanya kwa wanachi wake ni barabara ya Mbagala, Hospitali pamoja na Soko na ataingia chama chochote atakachoona kinamsingi mzuri.

Wasanii wengi wa Bongo Flava wameendelea kujiingiza kwenye biashara, 255 leo imepiga story na msanii 
Ruby ambae amesema anapenda kuwa designer, anatarajia kuja na kitu kinachoitwa
 ‘Kilemba cha Ruby’ ambayo inahusuana na mambo ya fashion, idea ambayo imekuja kutokana na kupenda kudesigne vilemba toka akiwa mdogo ingawa kipaji chake kikubwa ni kuimba.
 
 
No comments:
Post a Comment