KISA MSONGO WA MAWAZO WEMA SEPETU NA WOLPER WALEWA CHAKARI, WANASWA USIKU MNENE
Hatari! Masistaduu  wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline  Wolper Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa chakari, kisa  kikielezwa kwamba wana msongo wa mawazo, Risasi Jumamosi linafunguka.
Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe wakipiga mtungi usiku mnene.
ENEO LA TUKIO KINONDONI-MANYANYA
Tukio hilo  lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri hivi karibuni, usiku mnene  kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa kampuni ya Wema ya  Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye nyumba ya jamaa  mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa  kibao.
Katika pati hiyo ambayo  mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini, watu waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji.
Tofauti na ‘maraia’  wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga vinywaji vikali hadi wakawa  tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo ambalo liliwashangaza  wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo mastaa hao walivyozidi  kucharuka tofauti na walipofika kwani walionekana wapole na wastaarabu  kupita maelezo.
Baada ya ulabu kuwakolea walianza kupigana picha kwa simu kisha kukata mauno kabla ya Wolper  kuzimika kufuatia kuzidiwa na ‘kinywaji’.Kwa upande wake Wema alimpiga  vibao mwanaume shoga aliyetajwa kwa jina moja la Danny baada ya  kutibuana kabla ya watu kuwaamulia.Ulipofika muda wa kuondoka mahali  hapo, ilidaiwa kwamba Wolper ilibidi abebwe ili kupelekwa kwenye gari  kwani alikuwa hajiwezi.
Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper wakifurahia jambo.
KISA MSONGO WA MAWAZO
Uchunguzi wa Risasi  Jumamosi umebaini kwamba, mastaa hao wana msongo wa mawazo hivyo wanaona njia pekee ya kuwaondolea ‘stresi’ ni kunywa pombe.
WEMA
Habari za ndani  zilieleza kwamba, tangu Wema ameachana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu  Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa mtu mwenye mawazo na njia pekee ambayo  huitumia ni kujipooza kwa pombe kali.
“Ndiyo maana ana mpaka kaunta ya pombe kali nyumbani kwake,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu (Team Wema).
ZARI ATAJWA
Ilisemekana kwamba mbali na mawazo ya Diamond ambaye amehamia kwenye nyumba ambayo Wema alikuwa  na mchango mkubwa wakati wa ujenzi, pia suala la jamaa huyo kutanua na  mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ limekuwa likimpa  wakati mgumu mwanadada huyo.
Staa katika tasnia ya filamu, Bongo Wema Isaac Sepetu.
SUALA LA UGUMBA
Habari zilieleza kuwa,  jambo lingine linalompa Wema msongo wa mawazo ni suala la kukosa mtoto  kila anapomtafuta akiamini kuwa watu wanajua yeye ni mgumba.Pia  ilielezwa kwamba kuna suala la kuishiwa na kuogopa kufilisika kwani kwa  sasa filamu hazilipi na bado anataka kuendelea kuwa na heshima ya kuitwa Madam hivyo njia pekee anayoona inafaa kutuliza mawazo ni kunywa pombe.
WOLPER
Kwa upande wake Wolper  uchunguzi ulionesha kwamba, kwanza anapenda fedha hivyo kukosa tenda za  kuigiza na kuanguka kwa soko la filamu za Kibongo kumemsababishia msongo wa mawazo kama ilivyo kwa Wema kwani naye anataka kuishi maisha ya  kistaa ambayo hayawezekani bila kuwa na mshiko.
WOLPER KALOGWA?
Akizungumzia hali hiyo, Wolper alikiri kuwa na mawazo mengi huku akihisi kuwa huenda amelogwa.
USHAURI WA KISAIKOLOJIA
Staa katika tasnia ya filamu, Bongo Jackline Wolper.
Kwa mujibu wa mtaalam wa saikolojia aliyezungumza na gazeti hili juu ya mastaa aliwashauri kama ifuatavyo;
Mtaalam huyo alishauri  mastaa hao kuachana na pombe na kama wana mawazo ya kuumiza, wanatakiwa  kujilazimisha kutabasamu mara kwa mara na kusahau jambo linalowaletea  mawazo mabaya.
Alisema kuwa, kutabasamu kutawasaidia kuchangamsha akili, ingawa inaweza kuchukua muda kurudi  katika hali ya kawaida lakini inasaidia kuamsha hisia za furaha  zilizokuwa zimeshambuliwa na mawazo mabaya na kuamini katika ushindi.
WASISAHAU NYUMBA ZA IBADA
Pia aliwashauri kusahau  mambo yaliyopita na kujikita katika kufanya kazi kwa bidii hata kama  matunda hawayaoni sasa, yatakuja baadaye.Mbali na hivyo wajitahidi  kujichanganya katika makundi ya watu sahihi na kujumuika kwenye nyumba  za ibada, msikitini (kwa muislam) na kanisani (kwa mkristo).

















 

No comments:
Post a Comment