Recent Post

Friday, May 8, 2015

Salman Khan ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela, soma zaidi hapa




Muigizaji wa Bollywood Salman Khan ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela, kwa kumgonga na kumuua mtu kwa gari



Mahakama ya nchini India imemhukumu muigizaji wa Bollywood, Salman Khan kifungo cha miaka mitano jela kwa kumgonga na kumuua mtu asiye na makazi mwaka 2002 mjini Mumbai.

salman-khan._ready_hot_2012jpg

Mtu huyo alikuwa mmoja wa watu wengine watano waliogongwa kwenye tukio hilo. Muigizaji huyo alikuwa akikabiliwa na kosa la kuua bila kukusudia.

Khan alikuwa akijitetea kuwa ni dereva wake ndiye aliyekuwa kwenye usukani lakini jaji alisema muigizaji huyo alikuwa akiendesha gari mwenyewe na alikuwa amelewa.

Wataalam wa sheria wanaamini kuwa muigizaji huyo atakata rufaa.

Mawakili wa Khan wamekwisha omba dhamana kwa mahakama kuu ya Bombay ambayo itaisikiliza kesi hiyo.

Khan ni muigizaji wa kiume mwenye mafanikio sana nchini India na ameigiza filamu kama Dabangg, Ready, Bodyguard, Ek Tha Tiger, Maine Pyar Kiya na Hum Aap Ke Hain Kaun.




Email Newsletter



Smiley :)
:D
:)
:[
;)
:D
:O
(6)
(A)
:'(
:|
:o)
8)
(K)
(M)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Us

Contact Form

Name

Email *

Message *