By:  
Unknown
on 7:33 PM
Share
#Breaking: Maamuzi mapya baada ya Paul Makonda kukutana na madereva waliogoma !!
 Hii ishu ya mgomo wa mabasi ya abiria tangu mwaka 2015 umeanza imegonga vichwa vya habari kwa mara ya pili.. mara ya kwanza ilikuwa April 2015, lakini ukaisha baada ya kama saa 7 hivi kupita.
Hii ishu ya mgomo wa mabasi ya abiria tangu mwaka 2015 umeanza imegonga vichwa vya habari kwa mara ya pili.. mara ya kwanza ilikuwa April 2015, lakini ukaisha baada ya kama saa 7 hivi kupita. Jana May 5 2015 ikawa stori kubwa kwa mara ya pili, madereva wa mabasi wamegoma tena.. siku ikaisha huku kukiwa hakuna muafaka ambao umepatikana kuumaliza mgomo huo.
Jana May 5 2015 ikawa stori kubwa kwa mara ya pili, madereva wa mabasi wamegoma tena.. siku ikaisha huku kukiwa hakuna muafaka ambao umepatikana kuumaliza mgomo huo.
Leo tena hali ikawa kama jana, daladala na mabasi makubwa ya kwenda mikoani yote yaliendeleza mgomo.. ikafika saa sita mchana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda na Kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakaongea na viongozi wa Chama cha Madereva wakakubaliana na baadae mgomo ukaisha mabasi yakaanza safari.
Jahazi limeokolewa na viongozi hawa ambapo DC Makonda amewaahidi kwamba ameunda Tume ambayo itakutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kupata tamko la Serikali kuhusu madai ya madereva hao, na majibu yatapatikana kesho asubuhi kutoka Serikalini.


































 

No comments:
Post a Comment