WACHIMBAJI 19 WA DHAHABU WAFA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI KAHAMA
Eneo la machimbo  madogo ya  dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya  Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 
Mpaka sasa inadaiwa  wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya  kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na  kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo madogo ya  dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema waliofariki dunia ni  watu 19 ambapo usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivamia  machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa  imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na  kuwafukia na kusababisha vifo vyao. 













 

No comments:
Post a Comment