Ajali ya Hiace imeua watu 24 eneo la Uwanja wa ndege Kiwila Wilayani Rungwe  Mkoani Mbeya. Wadau Niko eneo la tukio, mpaka sasa miili 22 imefanikiwa  kutolewa. Kwani Hiace hii ilidumbukia mtoni na bado miili miwili  imenaswa, ndiyo inatolewa muda huu.
Watu wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta. Ajali hii imetokea wakati  Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela kugoma hivyo  baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria. Inaonekana ni ugeni Wa  barabara, speed na gari kukosa break za kuaminika
 
 
No comments:
Post a Comment