Recent Post

Monday, April 20, 2015

SERIKALI INAJIPANGA KUWARUDISHA WANANCHI WALIOPO AFRIKA YA KUSINI



TANZANIA YANUIA KUWAONDOA RAIA WAKE WALIOKO AFRIKA KUSINI     
Taswira za machafuko nchini Afrika Kusini, ambapo wenyeji wanawashambulia raia wa kigeni huku wakitakiwa wageni waondoke nchini humo.
Wenyeji wakifanya vurugu na kuchoma moto mataili.
Kufuatia kushamili siku hadi siku kwa mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini, Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa, inapanga kuwaondoa raia wake nchini humo.
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umesema umeanza zoezi la kuwatambua Watanzania waishio katika maeneo ya hatari nchini humo kabla ya kuanza hatua za kuwaondoa na kuwarejesha nyumbani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga, amesema kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepeleka maofisa wake katika mji wa Durban kuangalia hali ilivyo.
Kasiga ameongeza kuwa, serikali imeshatoa mwongozo wa namna ambavyo Serikali itawaondoa raia wake nchini Afrika Kusini.
Aidha amesema, utaratibu wa kuwaondoa Watanzania upo tayari, lakini si kila Mtanzania anayeishi Afrika Kusini ataondolewa, bali wale walio katika maeneo hatari na yanayosadikwa kushambuliwa na raia wenyeji wa Afrika Kusini.
Mamia ya raia wa kigeni wanaoishi Afrika Kusini wamekimbilia katika kambi zilizowekwa katika miji ya Johannesburg na Durban wakihofia maisha yao na hadi sasa raia sita wa kigeni wameshauawa katika mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yalishika kasi zaidi baada ya Mfalme wa Zulu, Goodwill Zwelithini kaBhekuzulu, kunukuliwa na vyombo vya habari mwezi uliopita akisema kuwa raia wa nchi za Kigeni wanapaswa kuondoka nchini humo.

Email Newsletter



Smiley :)
:D
:)
:[
;)
:D
:O
(6)
(A)
:'(
:|
:o)
8)
(K)
(M)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Us

Contact Form

Name

Email *

Message *