Muonekano wa gari la Mwamvita Makamba baada ya kurushiwa mawe na risasi South Africa.
Mwamvita Makamba ni mtoto wa Mzee Yusuf Makamba na ni dada wa Naibu Waziri January Makamba ambaye amekua akitajwa kwa uzito kwenye headlines za uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015.
Stori kwenye headlines hivi karibuni Mwamvita aliandikwa na baadhi ya magazeti kwamba baada ya January kutajwa kwenye headlines za uchaguzi mkuu, Mwamvita avamiwa na watu wenye silaha Johannesburg Afrika Kusini.
Baada ya hizo headlines kuendelea Mwamvita anaefanya kazi na kuishi Afrika Kusini alikubali kuongea kwenye Exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Hii haihusiani na January kugombea Urais na wala haihusiani na uvamizi unaofanywa kwa wageni Afrika Kusini, ilikua ni ajali tu imenikuta nikisafiri kutoka Johannesburg kwenda Sun city jioni’

>>> ‘Nilipita eneo ambalo mchana Polisi walituambia kulikua na maandamano kwahiyo jioni ile walikua wamebakia wahuniwahuni wachache lakini sisi hatukuona sababu ilikua usiku, wakati tunapita mbele yetu ndio tukaona vijana wamechoma matairi’
>>> ‘Nikajaribu kugeuza gari upesi ili nirudi tulikotoka lakini wale vijana wakaanza kutukimbiza, wakarusha mawe kwenye gari, mmoja akafyatua risasi lakini tuliweza kukimbia…. risasi na mawe yote yakagonga kioo changu cha nyuma cha gari ambacho ndio peke yake kimevunjika, tulikua wawili tu mimi naendesha na nilikua nimempa lift Mfanyakazi mwenzangu’
>>> ‘Lilikua ni tukio la dakika 5 tu lakini ilikua hatari sana sababu wale vijana wengine walikua wameshafika kwenye kioo changu pembeni yani walikua wameshalizunguka gari, tunamshukuru Mungu tuko salama na hakuna aliyejeruhiwa’ – Mwamvita Makamba
No comments:
Post a Comment