HALI ILIVYOKUWA NYUMBANI KWA GWAJIMA LEO
 Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.
 Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano. Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.
Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio. Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.
Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio. Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.
Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.   Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.  Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.
Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.  Baadhi ya waumini wa Gwajima wakifuatilia kwa makini hali iliyokuwapo.
Baadhi ya waumini wa Gwajima wakifuatilia kwa makini hali iliyokuwapo.  Baadhi ya waumini wakiwa mbele ya nyumba ya Gwajima.
Baadhi ya waumini wakiwa mbele ya nyumba ya Gwajima.  Gari la polisi likiondoka eneo la tukio.
Gari la polisi likiondoka eneo la tukio. Hapa wakishangilia ushindi baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
Hapa wakishangilia ushindi baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
WAKATI taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao  ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat  Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la  kumkamata askofu huyo lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.
Polisi hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo  maeneo ya Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo walipiga kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa  imefungwa kwa saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya  waumini wa askofu huyo kuruhusiwa kupita.
Hata hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na  viongozi kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri  kiongozi huyo afikie kituo kikuu cha polisi  kwa ajili ya mahojiano  zaidi ambapo alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu  ambapo taarifa za kina kuhusu kilichojiri huko zikiwa bado  hazijapatikana.















 

No comments:
Post a Comment