
April 02, ni siku ya Usonji duniani yani watoto wanaozaliwa hadi kufikisha miaka miwili lakini wanashindwa kuongea, mtangazaji 
Emmanuel Likuda amesema ameamua kujitolea kuwa balozi wa watoto wenye matatizo ya usonji, ambapo atafanya mambo mbalimbali ili kuhamasisha na kupeleka uelewa kwa watu kuhusu tatizo hilo kutokana na uelewa kuwa mdogo ambapo atafanya tamasha Tar 30, April 
Escape One.
 

Jana kwenye 255, msanii 
Darasa alisema haoni faida yoyote ya kufanya biashara ya kuuza mziki online akiongea kwenye 255, digital Meneja wa Mkito 
Ismail, ambao wanafanya kazi na
 Darasa amesema ili msanii apate mafao lazima awe na data base mzuri ya Social Network , kwasababu kipato kinategemea watu wanaofungua link ya wimbo wake na msanii anatakiwa afanye jitihada za kujitangaza mwenyewe na kuwataja
 Fid Q na 
John Makini kuwahi kufanya vizuri kwenye mauzo.
 

Mchekeshaji 
Stan Bakora amekuwa akimuigiza mwanamziki 
Nay Wa Mitego jinsi anavyoongea, amesema kuna siku walienda kwenye show 
Nay akamtanguliza watu hawakujua kama sio 
Nay kutoka na kushindwa kuwatofautisha sauti zao na anapenda kumuigiza kwasababu ya kupenda kazi zake.
 
 
No comments:
Post a Comment