Recent Post

Friday, April 17, 2015

WACHIMBAJI 19 WA DHAHABU WAMEFUKIWA NA KIFUSI, SOMA ZAIDI HAPA



WACHIMBAJI 19 WA DHAHABU WAFA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI KAHAMA     

Eneo la machimbo  madogo ya dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 

Mpaka sasa inadaiwa wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo madogo ya dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema waliofariki dunia ni watu 19 ambapo usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao. 

Email Newsletter



Smiley :)
:D
:)
:[
;)
:D
:O
(6)
(A)
:'(
:|
:o)
8)
(K)
(M)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Us

Contact Form

Name

Email *

Message *