TANZANIA YANUIA KUWAONDOA RAIA WAKE WALIOKO AFRIKA KUSINI
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umesema umeanza zoezi la kuwatambua Watanzania waishio katika maeneo ya hatari nchini humo kabla ya kuanza hatua za kuwaondoa na kuwarejesha nyumbani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga, amesema kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepeleka maofisa wake katika mji wa Durban kuangalia hali ilivyo.
Kasiga ameongeza kuwa, serikali imeshatoa mwongozo wa namna ambavyo Serikali itawaondoa raia wake nchini Afrika Kusini.
Aidha amesema, utaratibu wa kuwaondoa Watanzania upo tayari, lakini si kila Mtanzania anayeishi Afrika Kusini ataondolewa, bali wale walio katika maeneo hatari na yanayosadikwa kushambuliwa na raia wenyeji wa Afrika Kusini.
Mamia ya raia wa kigeni wanaoishi Afrika Kusini wamekimbilia katika kambi zilizowekwa katika miji ya Johannesburg na Durban wakihofia maisha yao na hadi sasa raia sita wa kigeni wameshauawa katika mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yalishika kasi zaidi baada ya Mfalme wa Zulu, Goodwill Zwelithini kaBhekuzulu, kunukuliwa na vyombo vya habari mwezi uliopita akisema kuwa raia wa nchi za Kigeni wanapaswa kuondoka nchini humo.
No comments:
Post a Comment