Unawajua watu ambao Rais wa FIFA Sepp Blatter anaofananishwa nao?
Blatter ameendelea kung’aa kwenye harakati za Uchaguzi huo.. huenda akashinda kwa mara nyingine baada ya wanachama kumi wa Shirikisho la soka Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kati na Muungano wa visiwa vya Carribbean (CONCACAF) kumuunga mkono kiongozi huyo katika uchaguzi mkuu.

Kitendo cha wanachama hao kufanya hivyo kimemfanya Blatter kufafanishwa na watu mashuhuri duniani walioweka historia na kujipatia umaarufu mkubwa kama Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela, Winston Churchill, Abraham Lincoln na Martin Luther King.
Rais wa CONCACAF, Jeffrey Webb amesema wanachama wake wanaendelea kumuunga mkono Blatter.
Wengine wanaowania Urais wa FIFA ni pamoja na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ureno Luis Figo, Mholanzi Michael van Praag, na Ali Bin Al Hussein
No comments:
Post a Comment