Hii ndio akiba ya ngoma za Beyonce zilizoko studio mpaka sasa!!
‘Xscape’ ni jina la album ya Marehemu Michael Jackson iliyoachiwa mwaka 2014, huu ni mfano wa jinsi ambavyo mastaa wa muziki wakubwa duniani huwa wanarekodi na kuhifadhi nyimbo zao studio, hiyo album ya Michael imeandaliwa wakati yeye ameshafariki.
Beyonce nae anaamini kwamba akiba haiozi, anahitaji kuuona muziki wake ukiishi muda mrefu, ukurasa huu unakusogezea hii story kwamba Producer wa muziki wa huyu dada, ambaye ni The Dream amesema kuwa akiba ya nyimbo za Beyonce ambazo ziko studio hajazitoa ni zaidi ya 100.
Album ya mwisho Bey kuiachia ilikuwa 2013 iliyopewa jina la ‘Beyonce‘, ambapo hiyo ni album yake ya tano.
No comments:
Post a Comment